Maswali na majibu

Hiki ni kiendelezi cha kivinjari cha Safari, kinaweza tu kuzuia matangazo ndani ya kivinjari cha Safari, SI ndani ya vivinjari vingine, programu au michezo. Ikiwezekana, tumia toleo la wavuti (yaani, fungua youtube.com kwenye kivinjari cha Safari).

Kivinjari cha Safari wakati mwingine hakipakii upya vichujio baada ya kusasishwa. Angalia ikiwa viendelezi vya programu bado vimewashwa kwenye Mipangilio, kisha lazimisha kuzima kisha uwashe upya kivinjari cha Safari (funga kisha ufungue upya).

Hapana. Programu inatumia API rasmi ya Uzuiaji wa Maudhui ya Apple - inatuma orodha ya kanuni za uzuiaji kwenye kivinjari cha Safari bila kufikia data yako ya kuvinjari.

Apple inaruhusu kiendelezi kimoja kutumia kanuni 50,000 za uzuiaji - kwa bahati mbaya hiyo haitoshi kwa programu za sasa za kuzuia matangazo. Hatua ya kuzigawanya katika viendelezi 6 inaruhusu programu kutuma hadi kanuni 300,000 kwenye kivinjari cha Safari.

Kwenye iOS/iPadOS gusa kitufe cha 'aA' kushoto mwa sehemu ya anwani na uchague kipengele cha 'Zima Vizuiaji vya Maudhui' ili kusitisha huduma ya uzuiaji kwa muda.
Kwenye menyu hiyo, unaweza kuchagua kipengele cha 'Mipangilio ya Tovuti' kisha uzime kipengele cha 'Tumia Vizuiaji vya Maudhui' ili kuzima huduma ya uzuiaji kabisa.

Kwenye macOS bofya kulia kwenye kitufe cha onyesha upya kulia mwa sehemu ya anwani na uchague kipengele cha 'Zima Vizuiaji vya Maudhui' ili kusitisha huduma ya uzuiaji kwa muda. Bofya kulia kwenye sehemu ya anwani na uchague kipengele cha 'Mipangilio ya Tovuti' kisha uzime kipengele cha 'Washa Vizuiaji vya Maudhui' ili kuzima huduma ya uzuiaji kabisa.

iOS/iPadOS:
Gusa kitufe cha 'aA' kilicho upande wa kushoto wa sehemu ya kuweka anwani. Chagua 'Mipangilio ya Tovuti' kisha uzime kipengele cha 'Tumia Vizuizi vya Maudhui'.
Ili uangalie na udhibiti orodha, nenda kwenye Mipangilio > Safari > Vizuizi vya Maudhui.

macOS:
Bofya kulia sehemu ya kuweka anwani, chagua 'Mipangilio ya Tovuti' kisha uzime kipengele cha 'Washa Vizuizi vya Maudhui'.
Ili uangalie na udhibiti orodha, nenda kwenye Safari > Mapendeleo > Tovuti > Vizuizi vya Maudhui.

1. Hakikisha kipengele cha Adblock Pro kimewashwa kwenye Mipangilio > Safari > Vizuiaji vya Maudhui (iOS) au Mapendeleo ya Safari > Viendelezi (macOS).

2. Fungua kipengele cha Adblock Pro na uwashe chaguo zinazopendekezwa kwenye kichupo cha kwanza.

3. Angalia orodha yako ya vipengee vinavyoruhusiwa na uone ikiwa hakuna data ya tovuti iliyoacha kuzuiwa.

Ikiwa hatua hiyo haifanyi kazi, zima kisha uwashe upya kifaa chako na urudie hatua za hapo juu. Jaribu tovuti nyingi, si tu ukurasa mmoja. Ikiwa bado unakumbwa na tatizo hilo, tafadhali tujulishe.

Huduma ya usawazishaji inatumika tu kwenye toleo la programu la 6.5 au jipya zaidi na toleo la iOS 13 au jipya zaidi na toleo la macOS Catalina (10.15) au jipya zaidi. Huduma ya usawazishaji inaweza kuchukua hadi dakika moja kukamilika. Ikiwa huduma ya usawazishaji inaonekana kuwa imekwama, wakati mwingine hatua ya kuzima kisha kuwasha upya programu inaweza kutatua tatizo hilo.

Ili kubadilisha kwa urahisi mipangilio kulingana na tovuti, unaweza kuweka kitufe cha kitendo cha programu kwenye kivinjari cha Safari. Kwenye iOS/iPadOS gusa kitufe cha shiriki kwenye kivinjari cha Safari, nenda chini kabisa, gusa kipengele cha 'Badilisha Vitendo...' na uongeze kitufe AdBlock Pro kwenye orodha.

JavaScript ni lugha maalum inayotumika kufanya tovuti zifanye kazi. Lakini wakati mwingine inaweza kutumiwa kuweka matangazo au kukufuatilia mtandaoni. Hatua ya kuizima itazuia shughuli hiyo, lakini inaweza kuathiri utendakazi wa tovuti pia.

Top